Mimi ni mshauri wa digital marketing, mjasiriamali na mwalimu kutoka Tanzania. Kwa miaka kadhaa nimesaidia wafanyabiashara kote Tanzania kuelewa jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia wateja na kukuza biashara zao.
Kutoka kujifunza digital marketing mwaka 2018, kushare tips zangu za kwanza mwaka mmoja baadaye, hadi kuona biashara zikigeuza mbinu zangu kuwa mauzo halisi.
Nilianza kujifunza mwenyewe digital marketing, mitandao ya kijamii, matangazo ya online na kutengeneza content.
Nilianza kushare online nilichokuwa najifunza. Tips za kuwaonyesha wafanyabiashara wengine kinachowezekana kwenye mtandao. Tabia ya kujifunza na kushare ikakua taratibu kuwa kazi yangu.
Mfanyabiashara mmoja aliniambia ameuza zaidi ya bidhaa 100 kutokana na tangazo moja la sponsored ads Instagram. Kwangu ulikuwa uthibitisho kwamba mbinu nilizokuwa najifunza na kufundisha zinaleta matokeo halisi kwenye biashara.
Biashara ya mteja wangu mmoja ilianza kuuza kwa wateja wa nchi jirani kupitia matangazo ya Meta. Kuona biashara ndogo ikivuka mipaka yake kulinithibitishia kwamba matangazo ya digital yanaweza kufungua milango iliyokuwa mbali kwa biashara ndogo.
Nilianzisha Optiza Digital, nikigeuza uzoefu wa miaka kadhaa kuwa agency inayosaidia biashara za Tanzania kukua kupitia mitandao ya kijamii.
Nina wafuasi zaidi ya 65,000 Instagram na 34,000 TikTok. Kozi yangu ya Uza Deilee imefundisha wanafunzi zaidi ya 1,500 mbinu za kuuza na kukuza biashara online.
Ujuzi wa digital unaleta fursa halisi za kiuchumi ukitumiwa vizuri. Leo naendelea kutengeneza content, kujenga digital products na kozi, na kufundisha marketing na ujasiriamali kwa watu wa Tanzania na nje ya Tanzania.
Safari yangu ni ukumbusho kwamba kazi inaweza kuanza na kitu rahisi kama kujifunza ujuzi na kushare unachokijua, na kukua kuwa kitu kikubwa zaidi.
Chagua njia inayokufaa: jifunze mwenyewe, tujifunze ana kwa ana, au nikurushie matangazo kwa niaba yako.